Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ratiba nzuri ya Darsa Maridhawa la "Subhi ya Kimaanawi" inaendelea kila siku asubuhi kwa Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa, Dar - es- Salam - Tanzania. Kipindi hiki ni fursa muhimu kwa wanafunzi kujipatia darsa za kiroho ambazo ni muhimu sana kwa Mwanafunzi yeyote kuhakikisha kuwa kabla ya kutafuta elimu anajikita kwanza katika kujiimarisha kiroho, kwa sababu elimu haiwezi kuwa na manufaa yoyote kwa mtu binafsi na kwa jamii nzima ikiwa mtu huyo hajaimarika kwanza kwa upande wa kiroho.
Elimu bila maadili ni upofu. Makusudio ya juu kabisa ya Elimu lazima yawe ni kumjenga Mwanadamu kitabia, kimaadili, kiadabu. Darsa hizi za kiroho ambazo kwa mujibu wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-Salam - Tanzania zinaitwa: "Darsa za Subhi ya Kimaanawi" zinamjenga Mwanafunzi na kumuimarisha katika upande wa adabu na maadili ya Kiislamu.
Hapana shaka kwamba kuna mahusiano makubwa kati ya elimu na adabu (maadili). Maulamaa wakubwa katika historia zao, walikuwa wakitafuta Adabu (Maadili) kwanza, kisha ndio wanaitafuta elimu. Wengine walikuwa wakiitafuta adabu kwa muda wa miaka 30, na elimu wanaitafuta kwa muda wa miaka 20. Kamwe hawakutanguliza elimu mbele ya darsa kama hizi za kimaadili. Na hii ndio Siri na Falsafa ya Ratiba ya Darsa ya "Subhi ya Kimaanawi" kwa Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa, Dar-es-Salam, Tanzania, ambapo hutangulizwa Darsa za Akhlaq (Adabu na Maadili ya Kiislamu) kabla ya kuingia Darasani ili kuchuma Elimu na Maarifa Safi ya Kiislamu.
Your Comment